Tovuti ya jumuiya ya Kibahá’í ya kiulimwengu
“Acha muono wako uwe ukumbatiao ulimwengu mzima…” — Bahá'u'lláh
Katika kipindi chote cha historia, Mungu amekuwa akituma kwa binadamu mfuatano wa Waelimishaji watakatifu—wajulikanao kama Wadhihirishaji wa Mungu—ambao mafundisho yao yametoa msingi kwa ajili ya uendelezaji wa ustaarabu. Wadhihirishaji hawa wamejumuisha Abraham, Krishna, Zoroasta, Musa, Buddha, Yesu Kristo, na Muhammad. Bahá’u’lláh, mtume wa sasa miongoni mwa Mitume hawa, alieleza kuwa dini za ulimwengu huja kutoka Chanzo kimoja na kwa asili ni kurasa zinazofuatana za dini moja kutoka kwa Mungu.
Wabahá'í huamini hitaji muhimu linaloikabili jamii ya binadamu ni kutafuta muono uunganishao wa jamii ya wakati ujao na wa asili na kusudi la maisha. Muono wa namna hiyo hukunjuka katika maandiko ya Bahá'u'lláh.
Asili ya Imani ya Kibahá’í na chanzo cha umoja wake wa kipekee.
Roho inayodumu milele, kusudi la maisha, na maendeleo ya sifa za kiroho
Mungu, ufunuo, binadamu, ulimwengu wa asili, na maendeleo ya ustaarabu
Ukuzaji wa mahusiano miongoni mwa watu binafsi, jumuiya, na asasi ambayo yanaakisi kanuni ya umoja wa binadamu.
Kanuni zinazohitajika kwa ajili ya upatikanaji wa amani na ujenzi wa ustaarabu mpya wa ulimwengu
Kusudi lenye malengo mawili ambalo ni la msingi kwa maisha ya Kibahá’í
Uunganishwaji wa huduma na ibada katika maisha ya jamii ya Kibahá’í.
Umuhimu wa familia na elimu ya watoto
Juhudi za vijana wa Kibahá’í kuchangia kwenye uboreshaji wa ulimwengu.
Maendeleo ya miundo ya kiutawala ya jumuiya ya Kibahá’í na uboreshaji wa michakato yake husika.
Kufanya kazi sambamba na wengine kwa uendelezaji mbele wa ustaarabu wa kimwili na wa kiroho