Katika kipindi chote cha historia dini kuu zimetoa kani ya msingi ya kuistaarabisha tabia ya mwanadamu, zinazosababisha kujinadhimisha, kujidhatiti na ushujaa kutoka kwa wafuasi wao. Kanuni nyingi za kimaadili ya kidini zimetafsiriwa katika miundo na ruwaza za tabia ambazo zimetumika kuinua uhusiano wa wanadamu na kuendeleza maisha ya pamoja ya jamii ya wanadamu.
Kila mara Mdhihirishaji wa Mungu anapojitokeza, kipimo kilichojaa zaidi cha upuzio kwa ajili ya hatua inayofuata katika uzindukaji na maendeleo ya jamii ya wanadamu kinaachiliwa katika ulimwengu. Mwanadamu—kiumbe wa kawaida kwa mtazamo wa nje—anaitwa kuwa msemaji mkuu kwa niaba ya Mungu. Mtu anaweza kumkumbuka Musa aliyesimama mbele ya Kichaka Kilichowaka moto, Buddha akipokea ujuzi chini ya mti wa Bodhi, Roho Mtakatifu akishuka juu ya Yesu katika umbo la hua, au malaika mkuu Jibril akija mbele ya Muhammad.
Katikati ya karne ya 19, Mungu alimwita Bahá’u’lláh—maana yake “Utukufu wa Mungu”—kufikisha Ufunuo mpya kwa jamii ya binadamu. Katika kipindi cha miongo minne, maelfu ya aya, barua na vitabu vilitiririka kutoka kwa kalamu Yake. Katika Maandiko Yake, Yeye aliandika muundo wa ukuaji wa ustaarabu wa sayari ambao hujumuisha sura zote mbili, ya kiroho na ya kimwili ya maisha ya binadamu.
Mimi Sijawahi kutamani uongozi wa kidunia. Kusudi Langu pekee limekuwa ni kuwafikishia watu kile ambacho Niliamriwa na Mungu kukifikisha…
— Bahá'u'lláh
Bahá’u’lláh aliteseka kwa miaka 40 ya kifungo, mateso na uhamisho kwa ajili ya kuleta ujumbe wa hivi sasa wa Mungu kwa jamii ya wanadamu. Leo, Maisha Yake na dhima vinaendelea kupata umaarufu kote ulimwenguni. Mamilioni ya watu wanajifunza kutumia mafundisho Yake katika maisha yao binafsi na ya pamoja kwa ajili ya uboreshaji wa ulimwengu.
Mafundisho ya Bahá’u’lláh…sasa yanatuwasilishia mfumo bora na safi kabisa wa mafundisho ya kidini...
— Count Leo Tolstoy, Mtunzi wa vitabu wa Kirusi