Ramani inayoonesha ukuaji wa Imani ya Kibahá’í kote ulimwenguni kama ilivyochorwa na Shoghi Effendi mnamo mwaka 1952.

Shoghi Effendi — Mlezi wa Imani ya Kibahá’í

Ili kuhakikisha kuwa Ufunuo Wake ungefanikisha azma Yake ya kujenga ulimwengu uliounganika—na kwa ajili ya kulinda umoja wa jumuiya ya Kibahá’í— Bahá’u’lláh alimteua Mwanae mkubwa kabisa wa kiume, ‘Abdu’l-Bahá, kama Kitovu cha Ahadi Yake na aliamuru uanzishwaji wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu. Kwa wakati Wake, ‘Abdu’l-Bahá alianzisha kanuni za kuendesha kwa ajili ya utendaji wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu na alisema kuwa baada ya kupaa Kwake, Wabahá’í lazima wamgeukie mjukuu Wake wa kwanza wa kiume, Shoghi Effendi, ambaye Yeye alimteua kuwa Mlezi wa Imani ya Kibahá’í.

‘Abdu’l-Bahá (kushoto) pamoja na mjukuu Wake wa kwanza wa kiume, Shoghi Effendi.

Vyote viwili, Nyumba ya Haki ya Ulimwengu na Mlezi walipewa jukumu la kutumia kanuni, kueneza sheria, kulinda asasi, na kuioanisha ipasavyo Imani ya Kibahá’í kuendana na mahitaji ya jamii iendeleayo daima .

Kwa kipindi cha miaka 36, kwa mtazamo usio wa kawaida, hekima na kujitoa, Shoghi Effendi kwa utaratibu wa hatua kwa hatua alilea maendeleo, aliongeza kina cha uelewa, na kuimarisha umoja wa jumuiya ya Wabahá’í, kadri ilivyoendelea kuakisi anuwai ya mbari nzima ya wanadamu.

Chini ya uongozi wa Shoghi Effendi, utaratibu wa kipekee uliotengenezwa na Bahá’u’lláh kwa ajili ya usimamiaji wa masuala ya jumuiya ulikua kwa haraka sana kila mahali ulimwenguni. Yeye alitafsiri Maandiko ya Kibahá’í kwenda lugha ya Kiingereza, alikuza kituo cha kiroho na kiutawala cha Imani katika Nchi Takatifu, na, katika maelfu ya barua alizoandika, alitoa umaizi wa kina katika sura ya kiroho ya ustaarabu na muundo wa mabadiliko ya kijamii, akifunua muono wa hamasa ya kustaajabisha wa siku zijazo ambao jamii ya binadamu inauendea.


Wote wanastaajabu kuona mafanikio yake makubwa mno na tabia yake ya uongozi, uongozi ambao ulitoa kwa watu wachache wa kawaida nguvu na uwezo ambao wao walikuwa hawajui kuwa wanao…

— David Hofman, mtunzi na mtangazaji

{{ note }}: